Shirika la Habari la Hawza, Wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali nchini Ufaransa walikusanyika kwa ajili ya kuwaunga mkono watu wanyonge wa Ghaza na kudai kumalizika kwa vita vya Gaza, na wakatoa wito kwenye vyuo vikuu na viongozi wa serikali kuzifikishia taasisi za kielimu nchini Israel matakwa yao haya.
Miongoni mwa madai mengine ya waandamanaji ilikuwa ni kwamba, mataifa yote yashiriki katika kampeni ya kuweka vikwazo vya kiuchumi dhidi ya utawala wa kizayuni unaomwaga damu, huku wakipaza sauti kauli mbiu yao isemayo "Palestina ni huru" na "Israil isusiwe," na pia walibeba mabango na maandiko yaliyoandikwa ujumbe wa aina hiyo.
Wanafunzi waliokuwa wakishiriki katika mgomo wa kula kwa siku tatu kwa ajili ya kuwaunga mkono watoto wa Palestina waliokumbwa na njaa, nao pia walikusanyika katika maandamano haya.
Lisa Greil, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 21, ambaye alikuwa mmoja wa washiriki, katika mazungumzo na shirika la habari la Anadolu alisema:
"Mara tu baada ya mkusanyiko huu kutangazwa nilijiunga haraka, na nimekuja hapa ili nipaze sauti yangu pamoja na wengine kwamba tunataka utekelezaji wa haki na ubinadamu huko Ghaza."
Mmoja wa waandaaji wa maandamano hayo pia alisema: "Israel inazuia kupelekwa msaada wowote wa kibinadamu kwenda Ghaza."
Na akaongezea kusena: "Kitendo hiki cha Israel ni mauaji ya kimbari ya wazi kabisa na ni usafishaji wa kikabila. Utawala huu ni wa kusikitisha."
Maoni yako